• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashabiki wa klabu ya Africain Tunisia wachangia zaidi ya $450,000 ndani ya siku moja kuokoa klabu yao

    (GMT+08:00) 2019-11-07 09:10:47

    Mashabiki wa klabu ya Africain ya Tunisia wamechangia zaidi ya $450,000 za Kimarekani ndani ya siku moja katika juhudi zao za kupambana kuokoa klabu hiyo inayokabiliwa na ukata, akiwemo shabiki mmoja asiyeona ambaye ameamua kusamehe pesa alizoweka kwa ajili ya dawa zake ili kuisaidia timu yake. Klabu ya Africain, ambayo ni klabu ya pili kwa ukongwe nchini Tunisia na ambayo ni maarufu sana katika Afrika imeondolewa pointi sita na kufungiwa kifedha kwasababu ya kutowalipa mishahara wachezaji wake wa zamani. Ili kuisaidia klabu hiyo, iliyoanzishwa mwaka1920, Shirikisho La Soka la Tunisia FTF liliunda kamati ya usimamizi wa sakata hilo ili kuokoa timu isijewekewa vikwazo zaidi. Oktoba FTF ilifungua akaunti kwa ajili ya mashabiki kuchangia pesa za kusaidia kulipa deni, ambayo hadi sasa imechangiwa $600,000 za Kimarekani. Kiasi cha jumla pamoja na mchango wa Jumanne uliokusanywa ndani ya saa 24, ina maana klabu sasa imechangisha zaidi ya dola milioni 1 ikiwa inajikongoja kulekea kwenye deni la jumla la $6m. Kampeni ya ndani ya saa 24, watoto walifika na visanduku vya kukusanyia pesa na shabiki asiyeona kukabidhi fedha zake za dawa, na badala yake walipata fulana zilizosainiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako