• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bingwa mara mbili wa Olimpiki Nicola Adams astaafu masumbwi kwa hofu ya kupoteza uwezo wa kuona

    (GMT+08:00) 2019-11-07 09:11:14

    Bingwa mara mbili wa Olimpiki Nicola Adams amestaafu mchezo wa masumbwi kwa hofu ya kwamba anaweza kupoteza uwezo wa kuona. Mbritania huyo mwenye miaka 37, amekuwa bingwa wa kwanza mwanamke wa Olimpiki baada ya kushinda medali ya dhahabu London 2012, na kuhifadhi taji lake la uzito wa kati katika Olimpiki ya Rio 2016. Ameanza kupigana ngumi za kulipwa 2017 na ni bingwa wa dunia wa WBO wa uzito wa kati. Adams amesema ameshauriwa kuwa akipata athari yoyote ile jichoni inaweza kumpelekea hatari ya kutoona kabisa. Pambano lake la mwisho lilikuwa Septemba 28 alipohifadhi taji lake la WBO alipopambana na Mmexico Maria Salinas. Amemaliza akiwa na rikodi ya ushindi mara tano na sare moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako