• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makubaliano ya RCEP ni makubaliano yenye sifa bora ya biashara huria

    (GMT+08:00) 2019-11-07 17:05:47

    Naibu waziri wa biashara wa China ambaye pia ni naibu mwakilishi wa mazungumzo ya biashara ya kimataifa Bw. Wang Shouwen amesema, Mkataba wa Uhusiano wa Wenzi wa Kiuchumi wa Pande Zote wa Kikanda RCEP ni makubaliano ya kiwango cha juu ya biashara huria, na kiwango cha ufunguaji mlango cha biashara ya mizigo kimezidi asilimia 90.

    Bw. Wang Shouwen ameeleza kuwa, mkutano wa tatu wa viongozi kuhusu Mkataba wa Uhusiano wa Wenzi wa Kiuchumi wa Pande Zote wa Kikanda RCEP uliofanyika hivi karibuni huko Bangkok, umetangaza taarifa ya pamoja ya viongozi hao.

    "Mkutano huo umetangaza rasmi nchi 15 wanachama zimemaliza mazungumzo, hali ambayo imeonesha kuwa ujenzi wa eneo hili la biashara huria lenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani, anuwai ya muundo wa wanachama, na mustakabali mkubwa zaidi wa maendeleo, limepata maendeleo makubwa."

    Mazungumzo ya RCEP yalianzishwa na nchi kumi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) mwaka 2012, China, na nchi sita zikiwemo India, Japan, Korea Kusini, Australia na New Zealand zilishiriki kwa mwaliko. Bw. Wang Shouwen ameeleza kuwa, nchi kumi wanachama wa ASEAN na nchi sita zilizoalikwa zimesaini kwa nyakati tofauti Makubaliano ya biashara huria "10+1", lengo lake ni kufikia Makubaliano mapya ya biashara huria yaliyo ya kisasa, ya pande zote, ya kiwango cha juu na ya kunufaishana.

    "Hayo ni makubaliano yenye sifa ya juu ya biashara huria. Kiwango cha ufunguaji mlango katika biashara ya mizigo kimezidi asilimia 90."

    Pia ameeleza kuwa, matokeo yaliyopatikana katika mazungumzo hayo yanazingatia ufuatiliaji wa maslahi wa pande mbalimbali. Amesisitiza kuwa China inaunga mkono umuhimu wa Jumuiya ya ASEAN katika mchakato wa mazungumzo.

    Bw. Wang ameeleza kuwa katika kipindi kijacho, ujumbe wa mazungumzo utaanzisha mara moja kazi ya ukaguzi na uthibitishaji wa nyaraka, ili kusaini makubaliano mwaka 2020. India bado ina masuala kadhaa ambayo yanahitajika kutatuliwa, pande mbalimbali ikiwemo China zitaendelea kudumisha majadiliano na India, na kuikaribisha ijiunge na makubaliano hayo mapema iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako