• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda yapinga masharti ya Uingereza ya kuwaachia waliokuwa maofisa wa jeshi

  (GMT+08:00) 2019-11-07 17:19:32

  Serikali ya Rwanda imekataa kuingilia kati katika kesi ya uhalifu inayohusisha waliokuwa maofisa wawili wa jeshi la Rwanda, ikiwa ni majibu ya barua iliyoandikwa na wabunge wa Uingereza kuomba watu hao waachiliwe huru.

  Mwaka 2016, aliyekuwa mlinzi wa rais Paul Kagame wa Rwanda, Kanali Tom Byabagamba, na Brigedia Jenerali Frank Rusagara, aliyekuwa mshauri wa kijeshi wa Rwanda kwenye ubalozi wa nchi hiyo nchini Uingereza, walikutwa na hatia na mahakama ya kijeshi mjini Kigali na kuhukumiwa kifungo cha miaka 21 na 20 kwa kuchochea vurugu kati ya wananchi na serikali na uongozi wa nchi hiyo.

  Jumatatu wiki hii, wabunge watano wa Uingereza waliandika barua wakiomba serikali ya Rwanda kuwaachia watu hao, wakisema afya zao si nzuri na wanahitaji huduma ya haraka ya matibabu maalum.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako