• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bunge la Afrika Kusini lapitisha muswada wa kurekebisha sheria ya ufadhili kwa masuala ya kisiasa

  (GMT+08:00) 2019-11-07 17:19:59

  Bunge la Afrika Kusini jana lilipitisha muswada wa marekebisho ya sheria ya kusimamia ufadhili wa mambo ya kisiasa.

  Msemaji wa bunge hilo Moloto Mothapo amesema, muswada huo, ambao utafanyia marekebisho Sheria ya Kuboresha Mfumo wa Kupata Taarifa (PAIA), unawaelekeza viongozi wa kisiasa kurekodi taarifa na kiasi cha pesa zinazotolewa na watu binafsi ama taasisi zinazozidi dola za kimarekani 6,739 katika mwaka wa fedha.

  Amesema chini ya sheria hiyo, viongozi wa kisiasa wanalazimika kuwasilisha rekodi hizo kila baada ya miezi minne, na kuzitunza kwa miaka mitano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako