• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shiboub aitwa Sudan, Kagere adai kukosa raha

  (GMT+08:00) 2019-11-07 18:00:15
  Mchezaji wa Simba, Sharaf Shiboub ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Sudan. Shiboub amejumishwa katika kikosi hicho ambacho kitacheza michezo miwili ya kufuzu AFCON 2021 dhidi ya Sao Tome Novemba 13 na Novemba 17 watacheza na Afrika Kusini. Wakati Shiboub akisafiri kuelekea Sudan kwa ajili ya kibarua hicho, mshambuliaji mwingine wa Simba Meddie Kagere amesema kuwa hakuna raha yoyote anayoipata kufunga mabao yake kwani anakamiwa na wapinzani mwanzo mwisho akiwa ndani ya uwanja. Kagere ni kinara wa ufungaji wa mabao ndani ya ligi kuu bara akiwa amefunga jumla ya mabao nane mpaka sasa kwenye michezo nane ambayo Simba imecheza.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako