• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bidhaa za teknolojia ya kisasa zaonyeshwa kwenye Maonyesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoingizwa China kutoka nje

    (GMT+08:00) 2019-11-07 19:15:25

    Bidhaa za matumizi za teknolojia ya kisasa zinazolingana na mahitaji ya watu zimewavutia watu wengi kuzitembelea katika Maonesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoingizwa China kutoka nje (CIIE) yanayofanyika mjini Shanghai, na kuonyesha wazo la "Teknolojia inabadilisha maisha".

    Kampuni ya Panasonic ya Japan imeweka kibanda chake kwenye jumba la maisha ya teknolojia, na imeonyesha bidhaa zenye teknolojia ya kisasa pamoja na ufumbuzi wake katika kutatua suala la uzee kwa watu na huduma ya matunzo ya uzeeni. Meneja mkuu wa tawi la kampuni hiyo nchini China Bw. Wu Liang amesema, maendeleo ya kasi ya China ni ishara kuwa mafanikio yanayopatikana kwenye soko la China yanahusiana moja kwa moja na maendeleo ya kampuni ya Panasonic. Amesema,

    "Biashara yetu nchini China inahusiana na maendeleo ya Panasonic katika miaka 100 ijayo. Mazingira ya kibiashara ya China yamekuwa mazuri zaidi kote duniani, nchi ambayo ina watu wengi wa tabaka la kati pamoja na ongezeko kubwa zaidi la pato la taifa duniani. Aidha, yapo makampuni 85 ya Panasonic na wataalamu zaidi ya 2,400 nchini China, hivyo sisi wafanyakazi zaidi ya elfu sita tunaamini kuwa tutafanya miujiza mipya nchini China."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako