• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Naibu waziri mkuu wa China atembelea timu ya madaktari wa China walioko Madagascar

  (GMT+08:00) 2019-11-07 19:17:59

  Naibu waziri mkuu wa China Bi. Sun Chunlan aliyeko ziarani nchini Madagascar, ametembelea hospitali ya Anosiala na kukutana na timu ya madaktari wa China wanaotoa huduma za matibabu katika hospitali hiyo, na kuzindua kituo cha Tiba ya Jadi ya Kichina cha China na Madagascar.

  Waziri wa afya wa Madagascar Bw. Julio Rakotonirina amesema, serikali ya nchi hiyo inashukuru uungaji mkono na misaada iliyotolewa na China kwa maendeleo ya afya na afya ya umma nchini humo. Amesema nchi hiyo itaimarisha ushirikiano na China kupitia fursa ya kuhimiza lengo la mpango mpya na kuhimiza ushirkiano wa afya kati ya nchi hizo mbili kuingia kipindi kipya.

  Kwa upande wake, Bi. Sun amesema, ushirikiano wa afya ni ushirikiano muhimu kati ya China na Madagascar, katika miaka 44 mfululizo China imewatuma madaktari 654 kwa Madagascar, na China ina nia ya kutekeleza pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" lililotolewa na rais Xi Jinping wa China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako