• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakulima wa pamba Tanzania walipwa Sh.bilioni 417

  (GMT+08:00) 2019-11-07 20:04:15
  Naibu Waziri wa Kilimo Tanzania,Hussein Bashe,amesema serikali imeshalipa Sh.bilioni 417 kwa wakulima wa zao la pamba nchini nzima na kwamba haitoingilia kupanga bei ya zao hilo ili kuhakikisha mkulima hapati hasara.

  Bashe aliyasema hayo jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza kutoka kwa mbunge wa Busega,Raphael Chegeni,ambaye alitaka kujua mkakati wa serikali wa kuwalipa wakulima wa pamba madeni yao ambayo wanaidai serikali.

  Bashe alisema serikali imehimiza kampuni zilizonunua pamba kuwalipa wakulima fedha zao na tayari Sh.bilioni 417 zimeshalipwa,na kiasi kinachodaiwa kwa sasa Sh.bilioni 50.

  Hata hivyo Bashe alikiri kuwapo kwa wakulima wa pamba ambao bado hawajalipwa pesa zao ,na kwamba sababu ya msingi ni kwamba asilimia zaidi ya 80 ya pamba inakwenda nje ya nchi.

  Alisema wanunuzi wanakabiliwa na msukosuko wa bei katika soko la dunia na wao kama nchi walitoa maelekezo ya bei ya kununulia kama serikali,ambayo ni maamuzi ya kumlinda mkulima asipate hasara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako