• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watendaji waiomba serikali kudhibiti teknolojia ya fedha

    (GMT+08:00) 2019-11-07 20:04:35
    Serikali ya Uganda inafaa kubuni mbinu za kudhibiti teknolojia ya fedha.

    Haya ni kulingana na Chama cha Teknolojia ya Fedha cha Uganda.

    Akizungumza katika tamasha la Africa Fintech Festival jijini Kampala jana,Mwenyekiti wa Chama cha Teknolojia ya Fedha cha Uganda,Peter Kawumi,alisema serikali inafaa kutoa muongozo kuhusu shughuli za kampuni za teknolojia ya fedha haswa kuhusu kutoa bei nzuri ya huduma zao.

    Alisema udhibiti huo utatoa muongozo katika sekta inayokua kwa kasi ambayo imerahisisha miamala ya fedha katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.

    Aidha aliongeza kuwa sekta hiyo inafaa kusaidiwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Habari na Teknolojia ya Uganda ili iweze kuzingatia viwango na utoaji wa huduma madhubuti.

    Kulingana na Bw Akiwumi,licha ya kuwa kuna Sheria ya Ulinzi wa Data na Faragha ya 2019,bado kuna haja ya serikali kuja na mfumo wa kanuni wa kuwalinda wateja

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako