• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yatafuta soko la kimataifa la maua

    (GMT+08:00) 2019-11-07 20:05:03
    Kampuni za maua nchini Rwanda zinalenga kupanua soko lao la kimataifa Rwanda kwa kushiriki katika Maonyesho makubwa ya Kimataifa ya Maua (IFTF).

    Maonyesho hayo,ambayo yameingia makala ya 10 sasa tangu kuanzishwa,yalifunguliwa jana nchini Uholanzi ,huku Rwanda ikishirikia kwa mara ya tatu sasa.

    Uholanzi ndio soko kuu la maua duniani na kwa kiasi kikubwa mchangiaji mkuu wa mauzo ya nje ya maua ya Rwanda (asilimia 98).

    Maonyesho hayo ya siku tatu yanaileta pamoja sekta ya maua duniani, ,huku yakilenga kuongeza uzalishaji na matumizi.

    Mwaka huu Rwanda inashiriki ikiwa na malengo ya kukuza sekta ya maua ya nchi hiyo.Matokeo yaliyokusudiwa ni athari chanya kwa mauzo na mahitaji ya maua ya Rwanda kupitia soko la mnada wa maua la Uholanzi.

    Sekta ya maua nchini Rwanda katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni imekua na kuvutia wawekezaji na soko kutokana na fursa na viungo vya soko kwa ajili ya bidhaa hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako