• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wahanga wote wa tukio la Essex wamethibitishwa kuwa ni raia wa Vietnam

  (GMT+08:00) 2019-11-08 08:40:58

  Wizara ya usalama wa umma ya Vietnam imethibitisha kuwa wahanga wote 39 waliokutwa wamekufa ndani ya lori katika kaunti ya Essex nchini Uingereza wamethibitishwa kuwa ni raia wa Vietnam. Wizara hiyo imesema watu hao wanatoka katika maeneo sita ya Vietnam.

  Waziri mkuu wa Vietnam Bw Nguyen Xuan Phuc ameiagiza wizara ya usalama wa umma ya Vietnam na mamlaka nyingine, kufanya kazi kwa karibu na mamlaka za Uingereza kushughulikia suala hilo, ikiwa ni pamoja na kutambua majina ya wahanga na kurudisha miili yao nyumbani.

  Serikali ya Vietnam imelaani vikali vitendo vya usafirishaji haramu wa binadamu na kutaka nchi mbalimbali kwenye kanda yake na dunia kuimarisha ushirikiano kuzuia vitendo hivi na kuwachukulia hatua za kisheria wahalifu wanaohusika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako