• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IAEA yathibitisha kuwa Iran imeanza kuhamishia Uranium kwenye kinu cha Fordow

    (GMT+08:00) 2019-11-08 08:41:19

    Shirika la nishati ya atomiki la kimataifa IAEA limethibitisha kuwa Iran imehamishia Uranium kwenye kinu cha Fordow.

    Msemaji wa shirika hilo amesema IAEA imethibitisha kuhamishiwa kwa uranium hiyo kutoka kwenye kinu cha Nantaz tayari kuwekwa kwenye mashinepewa mbili.

    Msemaji huyo amesema Kaimu mkurugenzi wa IAEA Bw Cornel Feruta ameripoti kwa bodi ya wakurugenzi ya shirika hilo kuhusu utekelezaji wa Iran wa makubaliano ya nyuklia (JCPOA) na hatua hiyo ya kuhamishia uranium.

    Jana IAEA ilisema Iran imeanza kuweka gesi kwenye mashinepewa kwenye kinu cha Fordow kilichoko kwenye handaki moja la mlimani kilometa 160 kusini mwa Tehran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako