• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan yatangaza mpango wa kufufua uchumi

  (GMT+08:00) 2019-11-08 08:43:45

  Serikali ya Sudan imetangaza mpango wa vipindi vitatu wa kutatua matatizo ya kiuchumi na kufufua uchumi wake.

  Tangazo hilo limetolewa na waziri wa fedha wa Sudan Bw. Ibrahim El-badawi, alipohutubia kikao cha Jukwaa la Washirika wa Kimataifa la Sudan SIPF, kilichofanyika jana Alhamisi mjini Khartoum.

  Mpango huo unalenga kutuliza uchumi, kutunga upya bajeti, kujenga amani, kutafuta ajira kwa vijana na kuiingiza Sudan kwenye mfumo wa kifedha wa kimataifa.

  Bw. El-badawi pia ametaja juhudi zilizofanywa na serikali kuiondoa Sudan kutoka kwenye orodha ya Marekani ya nchi zinazofadhili ugaidi.

  Akizungumza kwenye Jukwaa hilo, mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Gwi-Yeop Son amesisitiza ahadi ya Jumuiya ya kimataifa ya kuiunga mkono Sudan kutimiza malengo na vipaumbele vyake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako