• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yasema itafanya utafiti wa makini kabla ya kusaini mikataba yoyote ya uhamiaji

    (GMT+08:00) 2019-11-08 08:44:08

    Serikali ya Zambia imesema itafanya utafiti wa makini kabla ya kusaini itifaki na mikataba yoyote inayohusiana na uhamiaji.

    Waziri wa mambo ya ndani wa Zambia Bw. Stephen Kampyongo amesema Zambia itafanya uchunguzi wa kina kuhusu itifaki na mikataba inayoweza kuhujumu usalama na mamlaka ya nchi hiyo.

    Waziri huyo amesema Zambia inaunga mkono msimamo wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC kuwa matishio dhidi ya usalama na mamlaka ya nchi yoyote yanatakiwa kuzingatiwa wakati wa kusaini itifaki zinazohusika.

    Bw. Kampyongo amesema hayo nchini Ethiopia alipozungumza kwenye Kikao cha Mawaziri kwa ajili ya Mkutano wa tatu wa Kamati Maalumu ya Kiufundi kuhusu Uhamiaji, Wakimbizi wa ndani na nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako