• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchezaji soka aingia matatani kwa kuua kuku kiwanjani

    (GMT+08:00) 2019-11-08 08:53:59

    Watetezi wa haki za wanyama nchini Croatia wametangaza kumfungulia mashtaka mchezaji wa soka wa nchini humo aliyempiga teke kuku hadi kufa wakati wa mechi ya nusu fainali wikiendi iliyopita. Mchezaji soka, Ivan Gazdek kutoka timu ya nyumbani NK Jelengrad, aliwakimbiza kuku, na kumpiga teke mmoja wao kisha kumrembea nje ya uzio huku manyoya yake yakiwa yametawanyika. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 alipewa kadi nyekundu kwa tabia yake ya ukatili. Shirika lisilo la Kiserikali la Marafiki wa Wanyama pia limelaani vikali kitendo hicho cha aibu na cha woga dhidi ya kuku asiye na hatia aliyekufa akiwa amevunjika mifupa na kuwa na maumivu makali. Watetezi hao wamesema watamshtaki mchezaji kwa kosa la kuua mnyama au kutesa. Kama atashtakiwa kisheria na kupatikana na hatia, mchezaji huyo anaweza kufungwa jela mwaka mmoja. Gazdek, anayedai kuwa anapenda wanyama amesema hakuua kwa kukusudia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako