Katibu wa Chama Cha Ngumi Nchini Tanzania PCT, Antoni Rutha, amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi usiku wa pambano litakalofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Akizungumza na Waandishi wa habari, Ruta amesema katika kuelekea pambano hilo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ndiye atakuwa mgeni Rasmi. Kwa upande wa maandalizi kuelekea pambano hilo Ruta amesema yamekamilika na kwa Sasa Wana msubiri Arnel Tinampay kuwasili Nchini. Pambano la Mwakinyo na Tinampay linatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam huku mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |