• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan Kusini na kiongozi wa upinzani wakubaliana kuahirisha kuundwa serikali ya umoja

    (GMT+08:00) 2019-11-08 09:27:38

    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na kiongozi wa upinzani Bw Riek Machar wamekubaliana kuahirisha uundaji wa serikali ya umoja kwa siku 100.

    Taarifa iliyotolewa jana baada ya mazungumzo kati ya viongozi hao mjini Entebbe, Uganda inataja sababu ya kurefusha muda huo utakaoanzia Novemba 12 ni masuala muhimu kuhusu mambo ya usalama na utawala wa serikali bado hayaafikiana.

    Mazungumzo hayo yaliitishwa na rais Yoweri Museveni wa Uganda na mwenyekiti wa Baraza la Utawala nchini Sudan Bw. Abdel-Fattah Al-Burhan ambao ni wadhamini wa makubaliano yaliyosainiwa mwezi Septemba mwaka jana kuhusu utatuzi wa mapambano nchini Sudan Kusini. Mjumbe maalumu wa Kenya nchini Sudan Kusini Bw. Kalonzo Musyoka pia alihudhuria mazungumzo hayo.

    Kwa mujibu wa makubaliano hayo serikali ya umoja ingeundwa mwezi Mei mwaka huu, lakini pande zinazopambana zilikubaliana kuahirisha mpaka mwezi Novemba. Imefahamika kuwa tofauti kubwa zaidi ni mipaka ya mikoa na jinsi ya kuunganisha vikosi vya usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako