• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mtaalamu: Afrika Kusini ina nguvu ya kuvutia wawekezaji

  (GMT+08:00) 2019-11-08 09:28:05

  Wakati mkutano wa pili wa Baraza la uwekezaji la Afrika Kusini unafika mwisho, imefahamika kuwa mabilioni ya mitaji yanaonyesha kuwa nchi hiyo bado ina nguvu kubwa ya kuvutia wawezekaji. Hayo yalisemwa na mwanauchumi Jannie Rossouw, ambaye ni mkuu wa Chuo cha uchumi na biashara katika Chuo kikuu cha Witwaersrand. Mwanauchumi huyo ameongeza kuwa wawekezaji wa kimataifa wanataka kuwekeza nchini Afrika Kusini, hali ambayo ni tofauti na wakati rais Zuma alipokuwa madarakani.

  Rais Cyril Ramaphosa aliitisha mkutano huo kwa lengo la kukusanya dola za kimarekani bilioni 100 katika miaka mitano ijayo ikiwa ni juhudi zake za kufufua na kukuza uchumi wa Afrika Kusini ambao umekwama.

  Katika mkutano kama huo uliofanyika mwaka jana, wewekezaji waliahidi kutoa mitaji ya Rand bilioni 300, sawa na dola za kimarekani bilioni 20.3, na kwa mujibu wa rais Ramaphosa Rand bilioni 238 zimetumiwa kihalisi na Afrika Kusini. Mkutano wa mwaka huu ulikusanya mitaji ya Rand bilioni 363. Uwekezaji huo unatarajiwa kuleta nafasi za ajira zaidi ya laki 4.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako