• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU: Kupanua masoko ya ndani ya Afrika kunasaidia kuboresha mifumo ya uzalishaji barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-11-08 09:28:30

    Ripoti ya mwaka 2019 kuhusu maendeleo ya Afrika iliyotolewa na Umoja wa Afrika inasema, nchi za Afrika kupanua masoko ya ndani kunasaidia kuboresha mifumo ya uzalishaji.

    Ripoti hiyo iliyochapishwa Jumatano pia inasisitiza umuhimu wa kuharakisha mabadiliko ya kiuchumi barani Afrika kupitia ushirikiano mkubwa kati ya serikali na kampuni binafsi. Ripoti hiyo inasema, kampuni za Afrika ni ufunguo wa mabadiliko ya kiuchumi huku mazingira mazuri yanayoandaliwa na serikali yanachangia ukuaji wa kampuni hizo.

    Kwa mujibu wa ripoti, kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2018, wastani wa ongezeko la uchumi wa Afrika ulikuwa asilimia 4.6 ambao uliweka rekodi, ambapo mahitaji ya masoko ya ndani ya nchi za Afrika yalichangia asilimia 69 ya ongezeko hilo. Ripoti hiyo inatarajia kuwa mwaka huu uchumi wa Afrika utaongezeka kwa asilimia 3.6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako