• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wa Afrika washiriki kwenye Maonesho ya Pili ya Kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China kutoka nje CIIE

    (GMT+08:00) 2019-11-08 17:05:30

    China inaendelea kufungua soko kwa udhati kwa nchi mbalimbali, na kuendelea kuandaa Maonesho ya Kimataifa ya Uingizaji wa Bidhaa kutoka Nje ya China (CIIE), ili kutoa fursa kwa dunia kushiriki kwenye soko kubwa linaloandaliwa na China. Wakati wa maonesho hayo ya pili, uwezo mkubwa wa matumizi na mahitaji mbalimbali nchini China umezifanya bidhaa mbalimbali kutoka Afrika ziagizwe kwa wingi.

    "Hii ni yuan 230 kwa chupa, ile ni yuan 120 kwa chupa." "Ipi ina uwezo wa kuzuia ukame?" "Ni hii, yuan 80 kwa chupa."

    Kijana kutoka Uganda Jeninah Owomugisha anashiriki kwenye maonesho hayo akileta siagi ya parachichi na bidhaa za utunzaji wa ngozi ambazo zinatengenezwa na kiwanda chake. Ingawa kibanda chake kiko pembezoni, lakini wateja wengi wa China wanakitembelea, kwani kwa wateja wengi wa China, bidhaa kutoka Afrika zina umaalumu wa kutokuwa na uchafuzi.

    Hii ni mara ya pili kwa msanii wa uchongaji wa mawe kutoka Zimbabwe Tendekayi Tandi kushiriki kwenye maonesho hayo. Uchongaji wa mawe ni usanii wenye umaalumu wa Zimbabwe, ambao unapendwa sana na wateja wa Ulaya na Marekani. Katika miaka ya hivi karibuni, wateja wengi zaidi wa Afrika pia wanaupenda. Tandi anasema:

    "Nimepata wateja wanaopenda bidhaa yangu na kufanya ushirikiano wa muda mrefu kupitia maonesho ya kwanza yaliyofanyika mwaka jana. Mwaka huu nimeleta bidhaa zaidi ya mia mbili. Natumai kuwa nitapata wateja wengi zaidi wa muda mrefu, ili kuuza bidhaa za uchongaji wa mawe wa Zimbabwe nchini China."

    Bado wapo wafanyabiasara wengi kama Tandi ambao wanatafuta wafanyabiashara wanaoshughulikia uingizaji wa bidhaa kwa muda mrefu. Adane Demisse ambaye ni mfanyakazi wa Shirikisho la wafanyabiashara wa uuzaji wa kahawa la Ethiopia ni miongoni mwao.

    "Hapo awali niliambiwa kuwa mahitaji ya kahawa nchini China yanaongezeka, haswa vijana wa China wanapenda sana kunywa kahawa. Hivyo nimeshiriki kwenye maonesho haya kwa kuchukua mbegu ya kahawa."

    Maonesho haya yametoa fursa kwa bidhaa nyingi zaidi za Afrika kuuzwa nchini China, jambo ambalo si kama tu limehimiza biashara kati ya pande hizo, bali pia imeleta nafasi nyingi za ajira kwa watu wa Afrika. Kama waziri wa biashara na viwanda wa Zambia Bw. Christopher Yaluma alivyosema, maonesho hayo yamefungua njia nyingine ya kuendeleza uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako