• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa hatua 20 za kutuliza uwekezaji kutoka nje

    (GMT+08:00) 2019-11-08 17:27:35

    Baraza la Serikali ya China jana limechapisha "Mapendekezo ya kuboresha kazi za uwekezaji kutoka nje", zikiwemo hatua halisi 20 za kuweka mazingira mazuri ya kibiashara kwa makampuni ya nchi za nje, ambazo ni pamoja na kuhimiza ufunguaji mlango, kuongeza nguvu ya kuhimiza uwekezaji, kuimarisha mageuzi ya kurahisisha uwekezaji, na kulinda haki halali ya uwekezaji kutoka nje.

    Mapendekezo hayo yanaelekeza kuwa, China itaendelea kupunguza zaidi orodha ya sekta zilizozuiliwa kwa uwekezaji kutoka nje kuingia kwenye soko lililoko maeneo ya majaribio ya biashara huria, kuondoa vikwazo kwenye orodha hiyo, na kuhakikisha utekelezaji wa hatua za ufunguaji mlango. China pia itaondoa vikwazo dhidi ya sekta za benki za nje, makampuni ya hisa na makampuni ya utawala wa mfuko nchini China, na kuyaruhusu makampuni ya nchi za nje kuchukua asilimia zaidi ya 51 ya hisa kuanzia mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako