• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afisa wa polisi ashitakiwa kwa kumuua mchezaji wa mpira wa miguu

  (GMT+08:00) 2019-11-08 17:55:54

  Afisa wa polisi ameshtakiwa wa mauaji ya mchezaji soka wa zamani Dalian Atkinson ambaye alikufa baada ya kupigwa na nguvu ya umeme. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Aston Villa mwenye umri wa miaka 48, alikamatwa katika nyumba ya baba yake katika eneo la Telford, Shropshire, tarehe 15 Agosti 2016. Atkinson alianzia kucheza soka katika timu ya Ipswich Town kabla ya kuhamia Sheffield Wednesday, Real Sociedad, Aston Villa na Fenerbah├že nchini Uturuki. Anakumbukwa sana kwa kufunga goli katika mechi ya msimu wa mwaka 1992-93 wakati alipoupepeta mpira kutoka katikati ya uwanja kabla ya kumchenga golikipa wa Wimbledon katika eneo la penati na kuutingisha wavu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako