Timu ya soka ya Zimamoto imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Zanzibar baada ya kufikisha pointi 22 kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mafunzo katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan jana. Hatua ya Zimamoto kurejea katika nafasi hiyo kunawashusha KMKM ambao sasa watakuwa wa pili wakiwa na pointi 20 na JKU inashika nafasi ya tatu wakiwa na point 18. Mchezo huo ambao ni wa mzunguuko wa tisa wa ligi hiyo ulianza kwa taratibu kwa kila mmoja kuusoma mchezo wa mwenziwe.