• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Namibia na China kuimarisha ushirikiano kwa kutumia majukwaa ya Ukanda Mmoja na Njia Moja na FOCAC

  (GMT+08:00) 2019-11-08 18:30:05

  Namibia na China zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wao kupitia Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja ili kuboresha maendeleo ya uhusiano wao wa kina na ushirikiano wa kimkakati.

  Hayo yamesemwa na naibu waziri mkuu wa China Sun Chunlan ambaye yuko ziarani nchini Namibia, alipokutana na Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah. Bi. Sun amesema, China iko tayari kuendelea kuimarisha msingi wa kuaminiana kisiasa kutokana na kuheshimiana, kunufaishana, usawa na kunufaika kwa pamoja.

  Pia China iko tayari kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili wakati wa mikutano yao miwili mwaka jana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako