• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vijana wa Malawi washiriki kwenye mradi wa ICT wa Huawei nchini China

  (GMT+08:00) 2019-11-08 18:41:41

  Kundi la vijana 10 kutoka nchini Malawi wanakuja China kushiriki katika mradi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) inayofadhiliwa na kampuni ya mawasiliano ya China, Huawei.

  Vijana hao ni kundi la nne la Wamalawi wanaoshiriki kwenye mradi huo ulioanzishwa mwaka 2015.

  Akiwaaga vijana hao hapo jana mjini Lilongwe, Waziri wa Habari, Elimu ya Uraia na Teknolojia ya Mawasiliano Bw. Mark Botomani amesema mradi huo wa Huawei unabadilisha maisha na kuwatambulisha wanafunzi mfumo wa ngazi ya kimataifa wa ICT, mafunzo kwa vitendo na ujuzi. Ameongeza kuwa mradi huo unaendana na matarajio ya rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kwa vijana wa Malawi.

  Amesema serikali ya Malawi inachukulia maendeleo ya ICT kama kichocheo cha maendeleo ya ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako