• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Thamani ya biashara ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa ya China yaongezeka kwa asilimia 2.4

  (GMT+08:00) 2019-11-08 18:59:35

  Takwimu zilizotolewa na idara ya forodha ya China zimeonesha kuwa, katika miezi kumi ya mwanzo ya mwaka huu, thamani ya biashara ya uagizaji na uuzaji bidhaa nchini China imefikia dola za kimarekani trilioni 3.7 na kuongezeka kwa asilimia 2.4 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

  Katika kipindi hicho, thamani ya biashara kati ya China na Ulaya imefikia dola za kimarekani bilioni 6, na kuongezeka kwa asilimia 8.3, na thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imefikia dola za kimarekani trilioni 1 na kuongezeka kwa asilimia 9.4.

  Kwa upande wa makampuni, ongezeko la bidhaa zilizoagizwa na kuuzwa na makampuni binafsi ya China limezidi asilimia10 na kuchukua asilimia 42.4 ya thamani ya jumla ya biashara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako