• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta ya Madini, mawasiliano zimepiga jeki uchumi wa Tanzania.

    (GMT+08:00) 2019-11-08 19:23:18
    Uchumi wa Tanzania uliongezeka kwa asilimia 7.2 katika robo ya pili ya 2019 ikilinganishwa na asilimia 6.1 mnamo 2018.

    Kulingana na Ripoti ya Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Tanzania iliyotolewa hivi karibuni, ukuaji wa haraka wa bidhaa za ndani katika kipindi cha Aprili-Juni 2019 ilitokana na utendaji bora wa sekta za ujenzi, madini na mawasiliano.

    Sehemu kubwa kwa Pato la Taifa katika robo ya pili ya 2019 ilitokana na shughuli za viwango vya juu ambazo zilifikia asilimia 41.5, ikifuatiwa na shughuli za msingi kwa asilimia 32.9 na shughuli za sekondari zilikuwa na sehemu ndogo ya asilimia 25.7, kabla ya marekebisho ya kodi.

    Ujenzi ulirekodi ukuaji mkubwa zaidi wa asilimia 19.6 ikifuatiwa na uchimbaji madini na uchomaji asilimia 17.2 na habari na mawasiliano asilimia 10.3,

    Uchumi ulikua kwa asilimia 6.6 katika robo ya kwanza ya 2019 na serikali inatarajia ukuaji wa mwaka mzima wa Pato la Taifa kukua kwa asilimia 7.1 mwaka huu, kutoka asilimia 7 mwaka jana.

    Ukuaji huo ulitokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa ndani wa vifaa vya ujenzi kama saruji, chuma ambavyo hutumiwa katika ujenzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako