Zaidi ya wawekezaji 100 wa ndani na nje wameonyesha nia ya kuweka biashara zao kwenye mbuga ya viwandani ya Naivasha inayotarajiwa, maafisa wa kaunti ya Nakuru wamesema.
Serikali, mnamo Julai mwaka huu, iliteua ardhi ya ekari 9,000 eneo la Naivasha, Mombasa na Machakos kama Kanda Maalum za Uchumi (SEZs), kwani ilizidisha juhudi za kukuza viwanda.
Idadi ya makampuni ya ndani na wawekezaji wa kigeni kutoka nchi kama India, Ulaya, Merikani, Uholanzi, Uchina, Sri Lanka na Thailand tayari zimeonyesha nia ya kuanzisha uwekezaji muhimu katika ukanda wa uchumi.
Kampuni ambazo zitakuwa ndani ya ukanda huo zinatarajiwa kufurahia unganisho wa moja kwa moja wa nguvu ya umeme ya beu rahisi kutoka kwa kiwanda cha umeme cha Olkaria.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |