• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya pili ya CIIE yenye kiwango cha juu cha sayansi na teknolojia kuangazia siku za baadaye

    (GMT+08:00) 2019-11-08 20:07:05

    Maonesho ya Pili ya Kimataifa ya Uingizaji wa Bidhaa Kutoka Nje ya China (CIIE) yanaendelea mjini Shanghai, ambapo bidhaa nyingi mpya zenye kiwango cha juu cha sayansi na teknolojia zimeoneshwa kwa mara ya kwanza duniani au nchini China, na zimefuatiliwa sana washiriki wote wa maonesho hayo. Matunda hayo mapya ya sayansi na teknolojia duniani siyo tu yatabadilisha kwa kina maisha ya watu, bali pia yatatia nguvu mpya katika ongezeko la uchumi wa dunia na kuangazia siku za baadaye za binadamu…..

    Hivi sasa, duru mpya ya mapinduzi ya sayansi na teknolojia na mageuzi ya viwanda iko katika kipindi cha kihistoria cha kutimiza mafanikio makubwa, na hali mpya ya uchumi wa dunia pia inaendelea kujitokeza, huku sayansi na teknolojia na uchumi zikiungana kwa kina. Maonesho hayo yamekuwa jukwaa muhimu la utekelezaji, kwani katika maonesho ya kwanza ya CIIE, bidhaa, ufundi na huduma zaidi ya mia moja zenye kiwango cha juu cha sayansi na teknolojia zilioneshwa kwa mara ya kwanza duniani. Kwa kulinganishwa na maonesho ya awamu iliyopita, maonesho ya pili ya CIIE yamekuwa na kiwango cha juu zaidi cha sayansi na teknolojia. Kutoka vifaa vikubwa vya kiakili hadi vifaa vingi vya tiba vyenye kiwango cha juu zaidi, kutoka bidhaa husika za mtandao wa 5G hadi utatuzi mpya wa uchafuzi wa hewa, sayansi na teknolojia hizo zote zimewafanya watu kuhisi kuwa, siku za baadaye zimefika.

    Uvumbuzi wa sayansi na teknolojia ni nguvu ya kwanza ya kuhimiza maendeleo. Duru mpya ya mapinduzi ya sayansi na teknolojia na mageuzi ya viwanda vimeleta teknolojia mpya, hali mpya na mitindo mipya ambayo inahitaji ukaguzi wa soko la kimataifa na kubadilika kuwa nguvu ya kuhimiza ongezeko la kiuchumi. Bidhaa nyingi zinazooneshwa katika maonesho hayo zinalenga soko kubwa la China.

    Hivi sasa, China inaelekea kuwa na maendeleo yenye sifa ya juu na kukabiliwa na haja ya mageuzi ya viwanda. Wakati huohuo, China ina watu bilioni 1.4, ambao ni pamoja na kundi la watu milioni mia 4 lenye pato la wastani na matumizi yao yanaonesha mweleko wa kuongezeka.

    Kutokana na athari za hatua ya upande mmoja na kujilinda kibiashara, uchumi wa dunia unakabiliwa na shinikizo kubwa la kupungua, huku ukitaka kutafuta ongezeko jipya. Bidhaa zinazooneshwa kwenye maonesho haya zitaleta nguvu mpya kwa ukuaji wa uchumi wa dunia. Kama ikiwezekana kuondoa vizuizi vya ujuzi, teknolojia, watu wenye ujuzi, kuimarisha ushirikiano wa uvumbuzi, kunufaika kwa pamoja na matunda ya teknolojia, kuimarisha ulinzi wa hakimiliki za ubunifu, maonesho haya yenye kiwango cha juu cha sayansi na teknolojia yataleta siku nzuri za baadaye kwa watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako