• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Juhudi za kikanda zaendelea ili kukabiliana na makundi yenye silaha mashariki mwa DRC

    (GMT+08:00) 2019-11-09 17:05:19

    Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema nchi za kanda zinahamasishwa kukabiliana na makundi yenye silaha yaliyopo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambayo yamekuwa yakiathiri usalama wa kikanda kwa muda mrefu.

    Akiongea kwenye mkutano na wanahabari huko Kigali Rwanda, wakati anajibu kuhusu ripoti ya uwezekano wa operesheni ya pamoja dhidi ya makundi yenye silaha mashariki mwa DRC, rais Kagame amesema mikutano iliyoshirikisha nchi kadhaa na kufanyika nchini humo inalenga kuchanganya nguvu za kukabiliana na makundi yenye silaha, akisistiza kuwa nchi nyingi zimekubaliana na hilo. Amesema sasa wanajitahidi kuwafanya na wengine wakubali pamoja na kusonga mbele.

    Kagame amesema hayo wiki mbili baada ya maofisa waandamizi wa jeshi kutoka DRC na nchi jirani za Rwanda, Uganda, Burundi na Tanzania kukutana mjini Goma ili kutafuta ufumbuzi wa hali ya kutokuwa na usalama inayoathiri mashariki mwa DRC na nchi jirani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako