• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Rwanda akaribisha maonesho ya (CIIE) ya China

  (GMT+08:00) 2019-11-09 17:06:03

  Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema maonesho ya Pili ya Kimataifa ya Uingizaji wa Bidhaa Kutoka Nje ya China (CIIE) yanayofanyika hapa China ni kitu wanachokifurahia kila siku, kwani biashara ni muhimu kwa uchumi wa nchi na dunia.

  Akiongea na wanahabari mjini Kigali, Rwanda, Kagame amesema kwa Rwanda iwe juhudi za pande mbili au pande nyingi kama Eneo la Biashara Huria la Afrika AfCFTA linavyoileta Afrika na nchi za Afrika pamoja kushirikiana na jumuiya au nchi yenye uchumi mkubwa kama China, hilo ni jambo zuri na lenye faida na ni kitu wanachotaka kuona kinatokea.

  Rais Kagame pia amesema anatarajia kupitia maonesho hayo wataongeza faida ya Rwanda na Afrika kutokana na utaratibu wa biashara wa China, na kusisitiza kuwa Afrika na China ni lazima zihakikishe zinafaidisha pande zote mbili iwe baina ya nchi na nchi au kupitia Eneo la Biashara Huria la Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako