• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasisitiza ufumbuzi wa kisiasa ni njia ya kutatua suala la Syria

  (GMT+08:00) 2019-11-09 18:09:15

  Mjumbe maalum wa China anayeshughulikia suala la Mashariki ya Kati Bw. Zhai Jun jana alisisitiza kuwa, China siku zote inaona njia ya kutatua suala la Syria ni kutafuta ufumbuzi wa kisiasa, uhuru wa mamlaka na ukamilifu wa ardhi wa Syria vinapaswa kulindwa na kuheshimiwa, na mustakabali wa Syria zinapaswa kuamuliwa na watu wa Syria.

  Bw. Zhai Jun amefafanua kuwa, hali ya Syria imekuwa na mabadiliko mapya hivi karibuni, na mwelekeo wa ufumbuzi wa kisiasa umekuwa ukiongezeka. Hata hiyo, amesema mapambano bado yanaendelea nchini Syria, makundi ya kigaidi bado hayajaondolewa, na hali ya hivi sasa ya Syria inakabiliana na matatizo mengi.

  Pia alisema kuwa, China inauunga mkono Umoja wa Mataifa kuongoza usuluhishi wa suala la Syria na inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kutoa mchango katika kutatua suala la Syria mapema iwezekanavyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako