• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zaidi ya watu laki 5 wanagombea nafasi za uongozi kwenye serikali za mitaa Tanzania

  (GMT+08:00) 2019-11-10 16:39:25

  Zaidi ta watu laki 5.39 wamewasilisha fomu za kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

  Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Bw. Selemani Jafo, amesema watu hao laki 5.39 ni kati ya watu laki 5.5 waliochukua fomu. Watu waliorudisha fomu hizo ni asilimia 97.29, na wengine zaidi ya elfu hawajarudisha fomu kwa sababu zisizojulikana. Amesema kwa sasa serikali itatangaza watu wenye sifa ya kugombea nafasi hizo.

  Hata hivyo vyama vinne vya kisiasa ikiwa ni pamoja na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CAHDEMA, ACT-Wazalendo, Chama Cha Kijamii (CCK) na Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) vimetangaza kujitoa kwenye uchaguzi huo, vikitaja ukiukaji wa kanuni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako