• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yasema itatokomeza tatizo la ukeketaji kabla ya mwaka 2022

  (GMT+08:00) 2019-11-10 16:40:06

  Jumuiya ya wazee na viongozi wa dini ya Kenya wameahidi kuhakikisha kuwa vitendo vya ukeketaji nchini Kenya vitatokomezwa kabla ya mwaka 2022.

  Viongozi hao wamesema hayo kwenye mkutano na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mkewe Bibi Margaret Kenyatta mjini Nairobi, wakitoa ahadi ya kushirikiana na serikali kuu, serikali za kaunti na wadau wengine kueneza mwamko kwenye jamii zao na kuhimiza elimu na maisha bora ya msichana.

  Ahadi hiyo imetolewa na wazee kutoka kaunti 22 ambazo zimeathiriwa zaidi na tatizo la ukeketaji, na inaunga mkono ahadi ya Rais Kenyatta kutokomeza vitendo hivyo kabla ya mwaka 2022. Rais Kenyatta amezitaka wizara ya njia, elimu, afya na utawala wa umma kuongoza juhudi za serikali kukomesha ukeketaji katika sehemu zote za Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako