• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China apongeza kufunguliwa kwa baraza la mwaka 2019 la kimataifa la utawala wa sheria la China

  (GMT+08:00) 2019-11-10 16:44:37

  Baraza la mwaka 2019 la kimataifa la utawala wa sheria la China limefunguliwa tarehe 10 huko Guangzhou, rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa ufunguzi wa baraza hilo.

  Kwenye barua yake Rais Xi amesema kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa pamoja kunahitaji kulinda utawala wa sheria. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali kuweka mazingira mazuri ya utawala wa sheria, kujenga utaratibu wenye usawa, haki na wazi wa sheria wa uchumi na biashara ya kimataifa, kusukuma mbele maendeleo ya kiwango cha juu ya kujenga "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa pamoja, na kutoa manufaa makubwa zaidi kwa watu wa nchi mbalimbali. Amezitaka pande mbalimbali ziimarishe mawasiliano, kuzidisha maelewano na kuhimiza kuendeleza na kuboresha mfumo wa sheria husika, ili utawala wa kisheria uwe na umuhimu mkubwa zaidi katika mchakato wa kujenga "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako