Maonyesho ya pili ya kimataifa ya uagizaji bidhaa ya China yamefungwa leo mjini Shanghai, huku makubaliano ya biashara yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 71.13 yakifikiwa kwa manunuzi ya huduma na bidhaa kwa muda wa mwaka mmoja.
Makamu mkurugenzi wa Idara ya maonyesho hayo Bw. Sun Chenghai, amesema ongezeko hilo ni asilimia 23 ikilinganishwa na mwaka jana, na jumla ya nchi, sehemu na mashirika ya kimataifa 181 yalishiriki kwenye maonesho hayo, na zaidi ya makampuni 3,800 yalishiriki kuonesha bidhaa.
Maonesho hayo yamefanyika chini ya kaulimbiu ya "zama mpya, mustakbali wa pamoja" kuvutia wateja laki 5 wa ndani na nje.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |