• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazindua kazi ya kuhakiki wakimbizi

    (GMT+08:00) 2019-11-11 08:34:38

    Kenya imeanza operesheni ya mwezi mmoja ya kuhakiki wakimbizi, kwa lengo la kuwaondoa raia elfu 40 ambao wameandikishwa kwa makosa kama wakimbizi.

    Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Bw. Fred Matiang'i amesema serikali inatambua mazingira ambayo raia waliandikishwa kwa makosa kama wakimbizi, kwa kuwa wengi kati yao walitaka kupewa chakula bure, huduma za afya na elimu za bila malipo na fursa ya kupelekwa nje ya nchi.

    Waziri huyo amesema ingawa vitendo hivyo vimekiuka sheria na vinastahili adhabu, serikali imeamua kuwasamehe wale waliotenda makosa hayo, kwa sababu wengi kati yao walijiandikisha wakiwa watoto.

    Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, wasomali zaidi ya elfu 80 wamerudishwa makwao kwa hiari katika miaka mitano iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako