• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 382 wafariki barabarani nchini Botswana katika miezi kumi ya mwanzo ya mwaka huu

  (GMT+08:00) 2019-11-11 08:54:50

  Idara ya uchukuzi, barabara na usalama ya Botswana, amesema watu 382 wamefariki nchini humo katika miezi kumi ya mwanzo ya mwaka huu kutokana na ajali za barabarani, idadi ambayo imeongezeka kwa asilimia 9 ikilinganishwa na mwaka jana.

  Mkuu wa idara hiyo iliyo chini ya wizara ya uchukuzi na mawasiliano ya nchi hiyo Bw. Godwin Tlhogo, amesema vifo vingi vinavyosababishwa na ajali za barabarani vinatokana na makosa na uzembe wa binadamu, wakati serikali ya nchi hiyo ikianzisha kampeni ya kuimarisha usalama barabarani kabla ya msimu wa sikukuu.

  Amesema licha ya makosa na uzembe wa binadamu, baadhi ya ajali zinatokana na kupasuka kwa magurudumu, kwa sababu magari mengi yanayoingizwa kutoka nchi za nje kama Japan, bado hayajabadilishwa magurudumu yanayoweza kuhimili joto.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako