• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Vilabu vingine viwili vya England vyapigana vikumbo kumuwania Samatta

  (GMT+08:00) 2019-11-11 08:55:06

  Kufanya vizuri kwa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta katika mechi ya Ligi ya Mabingwa kati ya timu yake Genk dhidi ya Liverpool, kumezidi kumsafishia njia mshambuliaji huyo. Mwanzoni mwa wiki jana Samatta aliifungia Genk bao moja ilipofungwa mabao 2-1 na Liverpool kwenye uwanja wa Anfield. Sasa Newcastle na West Ham za England zimeonyesha nia ya kumnasa mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na Genk mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya DR Congo. Kabla ya kujiunga na Mazembe alichezea Simba iliyomsajili kutoka Mbagala Market. Samatta alikuwa mfungaji bora kwenye ligi ya Ubelgiji msimu uliopita akifunga mabao 15 na kuisaidia Genk kutwaa taji. Kwa sasa nahodha huyo wa Stars ana mabao 13 katika kampeni za msimu huu. Samatta alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa ndani wa Afrika mwaka 2015.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako