• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini na China zasaini makubaliano ya ushirikiano wa afya

    (GMT+08:00) 2019-11-11 09:11:51

    Ujumbe wa Kamati ya mambo ya afya ya mkoa wa Anhui wa China, umesaini makubaliano na wizara ya afya ya Sudan Kusini pamoja na Chuo Kikuu cha Upper Nile, kuhusu kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya afya .

    Ujumbe huo umeipatia dawa hospitali ya mafunzo ya Juba, ambako kikundi cha saba cha madaktari wa China kinatoa huduma. Kiongozi wa ujumbe huo wa China Bw. Shan Xiangqian, amesema makubaliano hayo mapya yatawawezesha madaktari wa China waendelee kuipatia Sudan Kusini huduma za matibabu bila malipo, pia yanaweza kuimarisha kunufaika kwa pamoja na ujuzi, ujenzi wa uwezo na programu mbalimbali za mawasiliano.

    Wakati huohuo, ujumbe wa China umesaini Hati ya Maelewano MoU na Chuo Kikuu cha Upper Nile kuhusu kutoa mafunzo na kuongeza uwezo wa madaktari wa Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako