• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kipa Mtanzania ang'ara

  (GMT+08:00) 2019-11-11 17:59:50

  Kipa raia wa Tanzania, David Kisu Mapigano, ameonyesha kiwango kizuri na kuisaidia Gor Mahia kuwafunga watani zao wa jadi AFC Leopards mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Kenya iliyochezwa jana Jumapili Novemba 10 kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi. Mechi kati ya Gor Mahia maarufu K'Ogalo dhidi ya AFC Leopards inayofahamika zaidi kama Ingwe imepachikwa jina Mashemeji Derby na mara nyingi huvuta hisia ya mashabiki wengi wa soka ndani na nje ya Kenya. Kisu alitua Gor Mahia katika dirisha kubwa la usajili mwaka huu akitokea Singida United na amekuwa kipa chaguo la kwanza akichukua nafasi ya Boniface Olouch.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako