• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonyesho ya pili ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa nje ya China yatoa jukwaa la mawasiliano kwa nchi za Afrika

  (GMT+08:00) 2019-11-11 19:16:56

  Maonyesho ya Pili ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa Nje ya China yaliyofanyika mjini Shanghai yamemalizika rasmi jana.

  Viongozi na wasomi kutoka nchi za Afrika Mashariki wamesema, maonesho hayo yametoa jukwaa maalumu kwa nchi mbalimbali kuonesha bidhaa zao na kufanya mawasiliano.

  Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema, hali ya sasa ya biashara ya dunia inabadilika mara kwa mara, na Rwanda inapenda kufanya ushirikiano na jumuiya iliyoundwa na nchi mbalimbali au nchi kubwa ya kiuchumi kama China, na kuzitaka nchi za Afrika kutumia fursa ya maonyesho hayo kuongeza biashara kati yao na China.

  Naye Msomi kutoka Kenya Bw. Stephen Ndegwa ameandika makala katika vyombo vikuu vya habari inayohusu matarajio ya Kenya kwa soko la China. Amesema, China ni moja ya marafiki wakubwa wa biashara wa Kenya, pia ni nchi muhimu iliyofanya uwekezaji wa moja kwa moja nchini Kenya. Maonesho hayo yanatoa jukuwaa na fursa nzuri kwa kuingia soko kubwa la China kwa Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako