• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Polisi wa Hong Kong watoa wito kurudisha utaratibu wa jamii

  (GMT+08:00) 2019-11-11 20:15:49

  Polisi wa mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong nchini China wamesema, mapambano ya kimabavu yametokea katika maeneo kadhaa mkoani humo. Kamanda wa polisi wa Hong Kong Bw. Kwok Pak-chung amesema, mapema leo, polisi mmoja alifyatua risasi ili kumzuia mtu mmoja kumnyang'anya bunduki katika eneo la mashariki mwa mkoa huo, Bw. Kwok amesema,

   "Tukio hilo limetokea kwa ghafla, mfanyakazi mwenzangu hakuweza kutoa onyo ndani ya muda huo mfupi. Kitendo chake kinalenga kulinda usalama na bunduki yake."

  Wakati huohuo, Mkurgenzi mkuu wa idara ya uhusiano wa umma ya polisi ya Hong Kong Bw. Tse Chun-chung amesema, mwanamume mmoja alipigwa na kuchomwa moto katika eneo la mlima wa Maan, baada ya kuwazuia watu kuharibu miundombinu. Mwanamume huyo amepelekwa hospitali lakini hali yake si nzuri. Bw. Tse pia amesema, polisi imewakamata watu 266 katika wiki iliyopita.

  "Kuanzia Jumatatu iliyopita hadi leo, polisi imewakamata watu 266 wenye umri wa kati ya miaka 11 hadi 74 wanaotuhumiwa kukusanyika bila ya ruhusu, kuficha silaha, kufanya uharibifu, kushambulia polisi na raia na kujaribu kuua watu."

  Bw. Tse ametoa wito jamii ya Hong Kong kutulia na kurejesha utaratibu wa jamii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako