• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yaunga mkono ujenzi wa mradi wa barabara kuu inayopita Sahara nchini Nigeria

    (GMT+08:00) 2019-11-12 08:42:46

    Kampuni moja ya uhandisi ya China imesema itaendelea kuunga mkono ujenzi wa mradi wa barabara kuu inayopita jangwa la Sahara nchini Nigeria, na kukamilisha kwa wakati mradi wake wa barabara katikati ya nchi hiyo.

    Mradi huo ni miundombinu ya ngazi ya bara inayopita Algeria, Chad, Mali, Niger, Nigeria na Tunisia. Lengo lake ni kuchangia maendeleo ya mawasiliano ya kibiashara kupitia barabara na kuhimiza mafungamano ya kikanda barani Afrika.

    Akizungumza na wanahabari kando ya Kikao cha 70 cha Kamati ya ufuatiliaji wa mradi huo, mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Uhandisi wa Bandari ya China CHEC inayotekeleza ujenzi wa sehemu muhimu ya mradi huo nchini Nigeria Bw. Zhang Wenfeng, ameutaja mradi unaoendelea kuwa ni "mradi unaohimiza mafungamano ya kimataifa kwa maeneo yote barani Afrika".

    Kwa mujibu wa mkataba, ujenzi wa mradi huo unatakiwa kukamilika ndani ya miezi 36, asilimia 15 ya fedha za mradi zinatolewa na serikali ya Nigeria, na asilimia 85 zinazobaki zinagharimiwa na Benki ya EXIM ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako