• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yawataka wananchi wake kutumia fursa za biashara za kanda ya Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2019-11-12 08:54:13

    Serikali ya Tanzania imewataka wananchi wake kutumia fursa za biashara za eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki kufuatia kupitishwa kwa itifaki ya soko la pamoja.

    Naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Damas Ndumbaro ameliambia bunge mjini Dodoma kuwa fursa zipo kwenye biashara, uwekezaji na ajira. Dk. Ndumbaro amesema wajasiriamali wadogo na wakubwa wa Tanzania wana nafasi ya kutumia soko la jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini wanatakiwa kufuata kanuni ikiwa ni pamoja na kanuni ya asili ya bidhaa zilizotengenezwa ndani ya jumuiya, ili kutofautisha bidhaa za eneo hilo na nyingine kutoka nje.

    Amesema utambuzi wa bidhaa zilizozalishwa Afrika Mashariki unakuwa rahisi, kama bidhaa hizo zimetengenezwa kabisa au kupatikana kwenye nchi moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako