• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afrika iko tayari kwa miradi ya uwekezaji ya mabilioni ya dola za Marekani

  (GMT+08:00) 2019-11-12 08:54:34

  Mkurugenzi wa Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) Bw Akinwumi Adesina amesema mjini Johannesburg kwenye mkutano wa siku tatu wa baraza la uwekezaji la Afrika unaoendelea nchini Afrika Kusini, kuwa Afrika iko tayari kufikia makubaliano yenye thamani ya mamilioni ya dola kwenye miradi mbalimbali.

  Bw. Adesina amesema licha ya kuwa uwekezaji barani Afrika una hatari zake, hatari hizo zinakuzwa na haziendani na hali halisi ya takwimu zinazoonesha faida zinazotokana na uwekezaji. Amesema kuongezeka kwa uchumi wa baadhi ya nchi za Afrika kunatia moyo, wakati benki ya dunia inasema kati ya nchi kumi zenye ongezeko la kasi zaidi ya uchumi duniani, sita ziko barani Afrika na hali hii inatokana na uwekezaji mzuri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako