• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Naibu waziri mkuu wa China akutana na rais wa Ghana

  (GMT+08:00) 2019-11-12 09:01:56

  Naibu waziri mkuu wa China Bibi Sun Chunlan ambaye yuko ziarani nchini Ghana, jana huko Accra alikutana na rais Nana Akufo-Addo na kufanya mazungumzo na makamu wa rais Bw. Mahamudu Bawumia.

  Bibi Sun amezitaka China na Ghana zizidishe uaminifu wa kisiasa, kuimarisha uunganishaji wa mikakati ya maendeleo na mabadilishano ya uzoefu wa utawala, kuhimiza uratibu wa kimataifa, na kukuza uhusiano kati yao chini ya mifumo ya ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

  Rais Akufo-Addo amesema Ghana inapongeza kanuni zilizotolewa na rais Xi Jinping kuhusu kujadiliana kwa pamoja, kujenga kwa pamoja na kunufaika kwa pamoja, na inapenda kushirikiana na China kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako