• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wazimbabwe washindwa kupata noti mpya

  (GMT+08:00) 2019-11-12 09:10:16

  Watu wa Zimbabwe wameshindwa kupata noti mpya zilizoahidiwa na benki kuu ya nchi hiyo, iliyosema zingeanza kutumika jana.

  Uchunguzi uliofanyika jana mjni Harare umeonesha kuwa watu wa Zimbabwe hawakupata sarafu ya dola 2 za kizimbabwe, na noti za dola 2 na 5 kutoka benki. Baadhi ya taasisi za kifedha za nchi hiyo zimethibitisha kuwa bado hawajapata sarafu au noti za aina mpya.

  Mwezi uliopita gavana wa Benki Kuu ya Zimbabwe Bw. John Mangudya alitangaza kutolewa kwa noti mpya ili kutatua suala la ukosefu wa fedha taslimu. Noti mpya zenye thamani ya dola bilioni moja za kizimbabwe zitaingia sokoni katika miezi sita ijayo, ili kuzuia mfumko wa bei.

  Habari kutoka benki hiyo imesema benki zote nchini humo zitapatiwa noti mpya, na wananchi wataweza kuzitumia kuanzia leo Jumanne.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako