• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Eliud Kipchoge awa miongoni mwa wanariadha watano kuwania Tuzo za Riadha Duniani mwaka 2019

  (GMT+08:00) 2019-11-12 09:10:50

  Eliud Kipchoge amekuwa miongoni mwa wanariadha watano waliofika hatua ya fainali kuwania Tuzo za mwaka 2019 za Riadha Duniani kwa upande wa wanaume. Mkenya huyo mwenye miaka 35, amekuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia marathon chini ya saa mbili kwenye mbio za Ineos 1:59 Challenge huko Vienna, Austria mwezi Oktoba. Kipchoge pia ameweka rikodi katika Marathon ya London kwa saa mbili, dakika mbili na sekunde 37 mapema mwaka huu. Wamarekani Sam Kendricks na Noah Lyles, Mganda Joshua Cheptegei, na Mnorwey Karsten Warholm mwanariadha anayeruka vihunzi nao pia wanawania tuzo hizo. Tuzo za Riadha Duniani kwa wanawake na wanaume zitatangazwa Jumamosi, Novemba 23 kwenye Tuzo za Riadha Duniani mwaka 2019 huko Monaco. Kura ya kuamua wanariadha watano wa mwisho ilimalizika Novemba 5, ingawa orodha bado haijatolewa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako